Monday, January 14, 2013

WANAKIJIJI WA MTAA WA KIPUNGUNI B WAMKATAA MWENYEKITI NA KUMTIMUA KWENYE KIKAO

Hawa ni baadhi tu ya wanakijiji kati ya wengi  waliokuwemo  kwenye mkutano wa kijiji cha Kipunguni uliokuwa ufanyike katika kata hiyo lakini ukahairishwa baada ya wanakijiji kumkataa Mwenyekiti huyo na kumtaka aondoke nje ya kikao hicho ili Mkutano uendelee. Zilikuwa zinasikika kelele zikisema kuwa hatumtaki mwenyekiti!! hatumtaki!! atoke, atoke na ndipo mwenyekiti akaamua kuahirisha kikao.

 Baadhi ya wanakijiji hao walizizungumzia baadhi ya sababu zinazowafanya wamkatae mwenyekiti kuwa ni, Amefanya Uchafu mwingi katika kipindi cha miaka mitatu alichokaa ikiwemo kuuza kituo cha Polisi Jamii kilichozinduliwa na Mama Komba, kuuza maeneo ya Serikali bila kushirikisha wanannchi na pesa zinaingia mifukoni mwake, kuanzia aingie Madarakani hajawahi kusoma Mapato na Matumizi. Sababu hizo zilitajwa na Mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho ambaye hakutaka jina lake liandikwe Mtandaoni.

Waandishi wa habari walipotaka kuongea na Mwenyekiti huyo, alikataa kuonyesha ushirikiano na kuondoka na kuingia kwenye gari lake akidai kuwa hata waandishi wa habari wanawatetea wanakijiji.

"Sitaki bwana hata nyinyi mpo upande wao sitaki, sitaki sitaki kwanza sogeeni niondoke zangu", alisema Mwenyekiti huyo huku akiingia kwenye gari lake na kutimua Mbio.
Mwenyekiti akijaribu kupunguza jazba za wanakijiji waliokuwa wanapiga kelele za Kumkataa.

Baada ya Kushindwa kuwatuliza alipandwa na hasira na kuanza kuongea kiukali zaidi aka ahirisha kikao na kusema kuwa ni mpaka hali itakapo kuwa shwari ndipo kikao kingine kitaitishwa. kushoto kwake ni Diwani wa kata hiyo Bw, Nyansika Motena, na kulia ni kaimu Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bw, Magige Makenge ambaye wanakijiji wanamtaka ashikilie nafasi hiyo.
 Bw, Makenge alianza kukaimu nafasi ya Mwenyekiti baada ya Mwenyekiti wake kusimamishwa kwa Muda kwa ajili ya kupisha uchunguzi unaoendelea baada ya wanakijiji hao kupeleka barua kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuwa hawana imani na Mwenyekiti wao na ndipo akasimamishwa.
Mwenyekiti alijifungia kwenye gari hili na kutimua mbio

Namba za gari hizi hapa

Huyu ndiye Mwenyekiti asiyetakiwa na Wanakijiji wake

Baada ya Mwenyekiti kuondoka, wanakijiji walimshika Kaimu mwenyekiti ili aendeleze kikao(Mmoja wa wanakijiji akimrudisha kaimu Mwenyekiti Bw, Magige Makenge ili akashike nafasi ya Mwenyekiti aliyeondoka)

Mwisho Diwani aliamua kuingilia kati na kuwataka wananchi watulie

No comments:

Post a Comment