Monday, June 17, 2013

UCHAGUZI WA UDIWANI

 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana ameibuka mshindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mianzini uliofanyika jana kwa kupata kura 1283, huku Mgombea wa Cuf akipata kura 494, Chadema wakiambulia kura 315 na ADC walipata kura 26, NRA kura 9 na Mgombea wa NCCR Mageuzi akiambulia kura 1. Bawji amemzidi mshindi wa pili kwa zaidi ya nusu ya kura.
 Mara baada ya matokeo kutangazwa na tume kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata, Wanachama wa CCM waliletewa matokeo yale na kusomwa na Mkurugenzi wa uchaguzi wao ambaye ni Katibu kata wa Mianzini wa CCM, Abdallah Kihuku mbele ya hadhara ya Wana CCM waliofurika katika ofisi za kata . Picha na Emmanuel Shilatu wa http//: www.ndgshilatu.blogspot.com
 Mshindi mteule wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana akiongea machache kwa Wana CCM mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi. Bawji anaziba nafasi iliyokuwa wazi kufuatia kifo cha diwani wa kata hiyo.

No comments:

Post a Comment