OFISI
YA S/KALI ZA MITAA,
MTAA WA KIVULE,
KATA YA KIVULE,
S.L.P 20950,
DAR-ES-SALAAM.
KUMB/MWLK/MT/KVL/MK/AUG/13. 17/18/2013
OFISI
YA KATIBU WA C.C.M,
TAWI
LA ……………………...
KATA
YA KIVULE
ILALA – DAR ES
SALAAM.
YAH: KUKUOMBA PAMOJA NA WAJUMBE WOTE
WA KAMATI YA SIASA MHUDHURIE KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO.
Tafadhali husika na kichwa cha habari hapo
juu.
Kwa wadhifa wako, kwa heshima kubwa unaombwa
uwataarifu wajumbe wote wa kamati ya siasa wa Tawi la……………………………..mhudhurie
kikao cha maandalizi ya mkutano wa Mtaa kikatiba, kikao hicho kitafanyika
kwenye ukumbi wa ofisi ya S/kali ya Mtaa
wa Kivule tarehe 24/08/2013 saa 8.00 mchana.
Wajumbe wa kikao hicho ni;- Uongozi wa
S/kali ya Mtaa na wajumbe wa kamati za siasa Matawi yote C.C.M Mtaa wa Kivule. Dondoo za kikao hicho ni maandalizi ya
mkutano wa Mtaa kikatiba, utakaofanyika tarehe 31/08/2013 saa 8.00 mchana
kwenye uwanja wa S/kali ya Mtaa wa Kivule.
Tafadhali njoo na vielelezo vya mipaka ya
Tawi la………………………………………….kwa ajili ya maandalizi ya ugawaji wa Mitaa ndani ya
Mtaa huu.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwako
binafsi na Ofisi yako kwa ujumla, na nawatakia utekelezaji wenye ufanisi katika
kazi hiyo.
Wako
katika Ujenzi wa Taifa,
J.
B. GASSAYA.
M/KITI
WA S/KALI,
MTAA
WA KIVULE
Nakala;-
·
Katibu
wa C.C.M Kata ya Kivule – Taarifa
No comments:
Post a Comment