Wednesday, August 28, 2013

MUHTASARI WA MKUTANO WA WANANCHI WOTE WA MTAA WA KIVULE ULIOFANYIKA TAREHE 30/03/2013.

HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA    OFISI YA SERIKALI  YA MTAA WA KIVULE

MUHTASARI WA MKUTANO WA WANANCHI WOTE WA MTAA WA KIVULE ULIOFANYIKA TAREHE 30/03/2013.

MAHUDHURIO.

JUMLA YA WAJUMBE 183 WALIHUDHURIA MKUTANO HUO ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA OFISI YA SERIKALI ZA MTAA WA KIVULE.
DONDOO  ZA  MKUTANO  WA  LEO:-
1.       KUFUNGUA MKUTANO,
2.       KUSOMA MIHTASARI MIKUTANO YA KANDA NA MTAA,
3.       YATOKANAYO NA MIHTASARI HIYO,
4.       WIZI WA MIFUGO UNAKERA,
5.       BARABARA KUTOKA KITUNDA KUJA KIVULE NI MBOVU,
6.       MENGINEYO/MATANGAZO,
7.       KUFUNGA MKUTANO.                                                                                                            
Dondoo na 1 :- KUFUNGUA  MKUTANO:-
Afisa Mtendaji wa Mtaa, alimkaribisha M/Kiti kufungua  mkutano baada ya wananchi kuridhia kwamba  ufunguliwe. Muda wa saa 9.00 alasili M/kiti alisimama na kuwasalimia kisha kuwashukru, hatimaye kuwakaribisha  wote katika mkutano huo wa kikatiba, alitamka mkutano huu ni halali na aliufungua rasmi.
Dondoo ya 2:-KUSOMA MIHTASARI YA KANDA NA MTAA:-
MEO alisoma mihtasari yote moja baada ya moja kulingana na mikutano ilivyofanyika katika kanda na Mtaa. Wajumbe waliokuwepo kwenye  mikutano hiyo waliikubali na kuipokea  mihtasari hiyo.
 Dondoo ya 3:- YATOKANAYO NA MIHTASARI HIYO:-
                     i.            MEO aliwaeleza wananchi kwenye mikutano ya kanda, KERO kubwa zilionekana kuwa ni:-
Miundombinu(barabara na vivuko),  Kukosa usafiri, Maji, Umeme, Wizi wa ng’ombe/mifugo, Ukosefu wa maeneo ya kujenga shule, Makaburi, Zahanati,  Mipaka ya Mtaa kutokuainishwa na H/mashauri, Mapori yasiyoendelezwa kuwa maficho ya wezi na wanafunzi, Ukubwa wa Mtaa na Uongozi wa juu kutokuja kusikiliza kero zao. M/kiti aliwaomba wananchi kuwa wafanye subira  kero hizo zitashughulikiwa na sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:- SERIKALI KUU,  TANROAD, HALMASHAURI, WAFADHILI NA WANANCHI. 
  
   ii.  Wananchi walihoji eneo la STENDI ni kwa nini hadi sasa magari ya ABIRIA  hayakwenda FRAME  KUMI,  kufuatia maazimio ya  mkutano wa tarehe 22/09/2012? M/kiti aliwambia  kuwa tatizo la magari kutokwenda FRAME KUMI,  niushabiki  wa baadhi ya watu, kuyazuia bila sababu ya msingi.  Mjumbe mmoja alipendekeza kuwa, kwa vile utekelezaji wa azimio la mkutano wa tarehe 22.9.2012 la kuamuru magari yote yaende FRAME KUMI umeshindikana, napendekeza kuwa  magari ya abiria yageuzie Stendi ya S/kali na mengine yageuzie FRAME KUMI. Wajumbe wote wa mkutano  waliunga mkono pendekezo hilo kwa kupiga KURA za kunyosha mikono yao juu, na hakuna aliyepinga hata mmoja.                                                                                                                                                            
Kuhusu Soko la Mtaa, mjumbe mwingine alipendekeza kuwa ni muhimu wachaguliwe wajumbe wa kamati jinsia ya (KE) watu wanne,  itakayoshirikiana na kamati ya zamani jinsia ya(ME) watu wanne, M/kiti aliwahoji wao wanasemaje juu ya pendekezo hilo? Wote walikubaliana na hili pendekezo . M/kiti aliwaomba wapendekeze majina ya  wajumbe wanne ambao watachaguliwa na kuungana na kamati ya zamani na kuweza kufanya uchaguzi wa UONGOZI wa SOKO. Wajumbe walipendekeza majina ya watu waliopigiwa kura za wazi, ambao ni:-
1.       SARAH  MABEJA (KE),
2.       SALMA  MRISHO (KE),
3.       ZAHARA OMARY MZEE (KE),
4.       LUKULENZIA JOSEPH (KE),
WAJUMBE WAKAMATI YA ZAMANI NI:
1.       WAIRANGA WAMBURA CHACHA (ME),
2.       ALLY  MOHAMED  MSUMI (ME),
3.       HAMISSI NASSORO MBONDE (ME),
4.       HASSANI CHAMBUSO (ME).

MAAZIMIO YA DONDOO NA 3:-
1.       OFISI ya S/KALI ya MTAA izishirikishe OFISI za:-  KATIBU TARAFA—UKONGA, OCD UKONGA na UONGOZI wa MAGARI ya ABIRIA yanayokuja  KIVULE ili yahakikishe kuwa yanaitumia STENDI ya KIVULE SOKONI, mengine yaende FRAME KUMI kama mkutano wa 30/03/2013 ulivyoazimia.
2.       OFISI ya S/KALI ya MTAA iziandikie OFISI za:-  KATIBU TARAFA UKONGA, OCD UKONGA na UONGOZI wa MAGARI ya ABIRIA  za kuwaomba watoe ushirikiano ili ZOEZI hili liweze kufanikiwa kama wananchi walivyoomba, ni vema K/TARAFA- UKONGA na OCD UKONGA waambatanishiwe kopi za muhtasari wa mkutano huo wenye MAAZIMIO hayo.
3.       Kuhusu SOKO, Kamati  ichague uongozi wao kiisha ikae vikao kwa ajili ya kuweka mikakati ya kuboresha soko. Mikakati hiyo iletwe kwenye uongozi wa S/kali ya Mtaa, ili uipitie kabla ya utekelezaji.
4.       M/kiti aongozane na wajumbe  walioteuliwa na mkutano huu ili kufuatilia KERO kwenye OFISI za:- MH: MBUNGE JIMBO la UKONGA, SUMATRA, TANESCO, MANISPAA na DC. ILALA.   
DONDOO NA 4:- WEZI NI KERO KUBWA:-
 Wananchi wengi walionyesha kuchukizwa na wezi wa mifugo waliokithiri kwa kasi katika Mtaa wetu. M/kiti alisimama na kuwambia wajumbe wa mkutano kuwa tatizo hilo la wizi kama wakitaka litakwisha, ebu anzeni ulinzi shirikishi kwa kujilinda wenyewe ama kutoa michango kwa ajili yakuwalipa walinzi wa POLISI JAMII,  baada ya mjadala mrefu:-
 MAAZIMIO YA DONDOO NA 4:-
1. Wananchi wamekubaliana kuwa waanzishe VIKUNDI VYA POLISI JAMII kila KANDA.
2. Wizi ukitokea mkutano wa DHARURA uitishwe kwenye eneo la tukio mara moja. 
3. Kila kanda ifanye mkutano wa hadhara kwa ajili ya kuwatambua wezi kwa kuwapigia kura za siri.
4. Tunaomba kituo kikubwa cha POLISI kijengwe katika eneo lililotolewa  kwa ajili ya kazi hiyo.
5. Wenye maeneo/mapori yasiyoendelezwa/safishwa,  wayahudumie ili  yasiwe MAFICHO ya wahalifu wa usiku na mchana.

DONDOO NA 5:-BARABARA YA KITUNDA KIVULE NI MBOVU SANA:-
M/kiti alielezea ubovu wa barabara hiyo,  dondoo hii  ilichangiwa na watu wengi , hata wengine wakitoa ushuda wa madhara waliyoyapata kutokana na ajali zilizosababishwa na ubovu wa barabara hiyo.
MAAZIMIO  KATIKA DONDOO NA 5:-   
1.Wajumbe kwenye MKUTANO huo, waliazimia kuwa M/kiti wa S/kali Mtaa, afuatane na wajumbe watakaoteuliwa leo,  kwenda katika OFISI za:- MH: MBUNGE,  SUMATRA, TANESCO, DC- ILALA, K/TARAFA  na  MKURUGENZI-ILALA kufutilia utatuzi wa KERO hizo za wananchi.
2. Majina ya watu waliopendekezwa  kwa ajili ya kufuatana na M/Kiti wa S/kali ni:-                                                     
1.       ELIUS  NYANKENA  RAWE,
2.       KASSIMU A. NDOGORO,
3.       ZAHARA  OMARY  MZEE,
4.       ERASTO NJOWOKA.   

 DONDOO NA 6:- MENGINEYO/ MATANGAZO:
1.       MEO alitangaza taarifa ya mkutano wa baraza la katiba la wilaya kuwa utafanyika  siku ya tarehe 03/04/2013 saa 3:00 asubuhi  Ofisi ya S/kali ya Mtaa.
2.       Wananchi  waliwaombwa  wafanye usafi  wa mazingira yao kwani  ni machafu sana.
3.       Mjumbe mmoja aliomba afahamishwe kama MH: MBUNGE Eugin Mwaiposa ametekeleza zile ahadi alizoahidi siku ile uzinduzi wa TOVUTI Mtaa? Alitaja kuwa baadhi ya ahadi hizo ni:-
-MADAWATI 100 ya S/M KIVULE na S/M BOMBAMBILI.
-TOVUTI kwa ajili ya MTAA na.
-KULIMA BARABARA ya KITUNDA-KIVULE kwa kiwango cha CHANGARAWE. Aliambiwa kuwa majibu kamili yatapatikana baada ya kutoka OFISINI kwake na  ujumbe uliochaguliwa kufuatana na M/KITI kufuatilia kero za wanakivule.
MAAZIMIO YA DONDOO NA 6:-
1. Mkutano wa kupata wajumbe wa katiba utafanyika  tarehe 03/04/2013 kwenye viwanja  vyaS/kali za Mtaa wa Kivule saa 3.00 asubuhi.
2. Wananchi kufanya na kuchangia usafi kwenye maeneo yao.
3. Majibu yatapatikana baada kufuatiliwa katika ofisi husika.
DONDOO NA 7:- KUFUNGA MKUTANO:-
 M/kiti aliufunga mkutano saa 12:00 jioni kwa kuwashukru na kuwatakia afya njema wajumbe wote.

                                       IMETOLEWA NA 
                       M/KITI S/KALI/AFISA MTENDAJI

                                 MTAA WA KIVULE                                                                                                             Website: www.mtaawakivuletz.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment