Tuesday, March 26, 2013

MUHTASARI WA KIKAO CHA SERIKALI YA MTAA WA KIVULE KILICHO FANYIKA JUMATANO TAREHE 20/02/2013.




MAHUDHURIO.
1.    JOSEPH  B. GASSAYA                                                          M/KITI………………………..
2.    HEMEDI  A. NYUNGURU                                                      KATIBU………………………
3.    FRORA  G. BONIFACE                                                         MJUMBE……………………...
4.    ALLY  M. MSUMI                                                                  MJUMBE……………………...
5.    GRACE  M. KERANG’ANI                                                    MJUMBE……………………...
6.    JOHN  M. MESANGA                                                                       MJUMBE……………………...
KWA TAARIFA.
1.    JULIUS  M. GERULA                                                AFSA MTENDAJI WA MTAA
2.    ELIAS  KOROSO WAMBURA          -                                   MJUMBE

AJENDA ZA KIKAO.
1.    KUFUNGUA KIKAO.
2.    KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHOPITA.
3.    YATOKANAYO NA MAAZIMIO YA MUHTASARI.
4.    KUBADILISHA HATI ZA MAUZIANO.KWA WAKAZI WA KIVULE.
5.    DIRA YA KAZI ZA VIONGOZI WA KANDA ZA MTAA HUU.
6.    KUJADILI BARUA ZA WANAFUNZI YATIMA WA MTAA HUU.
7.    KUSOMA NA KUJADILI BARUA YA MAOMBI KUMILIKISHWA SILAHA.
8.    KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI MALORI YA MCHANAGA YAPITAYO KIVULE.
9.    KUFUFUA STENDI NA SOKO LA MTAA WA KIVULE..
10.  KUPANAGA TAREHE NA DONDOO ZA MKUTANO WA MTAA KIKATIBA.
11.  KUJADILI JINSI YA KUONDOA KARAKANA  BUBU SEHEMU YA STENDI YA KIVULE.
12.  MH: DIWANI  KATA YA KIVULE, ANAVURUGA MAENDELEO YA MTAA KWA KUSHINDWA KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI WA MTAA WA KIVULE.
13.  KUFUNGA KIKAO.
DONDOO NA 1. KUFUNGUA KIKAO.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule amefungua kikao kwa kusalimiana na wajumbe saa 4:29 asubuhi.


DONDOO NA 2. KUSOMA MUHTASARI WA KIKAO KILICHO PITA..
Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kivule Ndugu J. B. Gassaya aliwaeleza wajumbe kuwa muhtasari wa kikao kilichopita hautasomwa kwa vile aliyekuwa katibu wa kikao hicho ndugu Julius Gekula bado anaendelea na matibabu Hospitalini. Wajumbe walikubali kwa kauli moja na kuiacha dondoo hiyo hadi katibu atakapo rudi Ofisini.
DONDOO NA 3. YATOKANAYO NAMUHTASARI HUO.
Mwenyekiti aliwaeleza wajumbe yatokanayo  na kikao kilichopita hayapo, kutokana na sababu zilizoelezwa katika dondoo Na 2.
DONDOO NA 4. KUBADILISHA HATI ZA MAUZIANO KWA WAKAZI WA KIVULE.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule aliwaeleza wajumbe kuwa kwa sasa, Hati zinazotumika kwa ajili ya mauziano ya mashamba, maeneo,nyumba nk zimezagaa sana kwa watu ambao si waaminifu maana huwadanganya wateja wao kwa kutumia Hati hizo. Kwa usalama wa Mtaa wetu ni muhimu tubadilishe Hati mbadala ikiwa ni pamoja na kuwa na www.mtaawakivuletz.blogspot.com. Ambayo ni TOVUTI ya Mtaa wa Kivule.
 Mwenyekiti aliwaonyesha Hati ya Mauziano,ambayo ni mbadala. Wajumbe waliipitia na kwa kauli moja walikubali Hati hiyo mpya ianze kutumika na zile za zamani zichanwe na kuondolewa kwenye matumizi ya Kiofisi. Wananchi wataarifiwe,na atakayeigiza Hati hii mpya uongozi wa S/kali ya Mtaa huu utamfungulia mashtaka KISHERIA.
DONDOO NA 5. DIRA YA KAZI ZA VIONGOZI WA KANDA ZA MTAA WA KIVULE.
1.     KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA WA WAKAZI WA KANDA NA MALI ZAO.
2.     KUHAMASISHA WAKAZI KUHUDHURIA VIKAO/MIKUTANO NDANI YA MTAA NA KANDA HUSIKA.
3.     KUHAMASISHA WAKAZI KUCHANGIA NA KUFUATILIA SHUGHULI ZOTE ZA MAENDELEO, IKIWA NI PAMOJA NA VIKUNDI VYA ULINZI SHIRIKISHI, UJASIRIAMALI, MICHEZO NK.
4.     KUZUIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA, KAMA VILE UFUGAJI HOLELA,
 UCHIMBAJI/UCHIMBISHAJI MCHANGA, UJENZI HOLELA, UZIBAJI WA BARABARA ZA MITAA, UVAMIZI WA MASHAMBA/VIWANJA VYA WATU NK.
5.     KUTOA TAARIFA YA MATUKIO YOTE YA KIMAENDELEO AU KIUHALIFU KWA UONGOZI WA S/KALI YA MTAA, NA UWE UNATOA USHIRIKIANO WA HALI YA JUU SANA KWA UONGOZI HUO.
6.     NI MARUFUKU KUFANYA SHUGHULI ZOZOTE ZA KIUTENDAJI/KIUTAWALA NDANI YA KANDA BILA IDHINI/RUKSA YA UONGOZI WA S/KALI YA MTAA.


DONDOO NA6.KUJADILI BARUA YA WANAFUNZI YATIMA WA MTAA WA KIVULE..
Mwekiti wa S/kali ya Mtaa wa kivule aliwaeleza wajumbe kuwa kuna maombi yaliyoletwa  na wanafunzi/yatima kuomba kupata msamaha wa karo, wanafunzi/yatima hao ni.
1.    AMON JAHANSEN RWEGASIRA ------------YATIMA.
2.    MICHAEL AMOS--------------------------           ----------YATIMA.
3.    MATHAYO AMOSI--------------------------------- YATIMA.
Wajumbe baada ya kusomewa barua hizo za maombi, waliyajadili na kuazimia kuwa.
1.    .Hao wanafunzi/Yatima wote wasamehewe karo,  
2.    Uongozi wa Mtaa uwaandikie barua ambayo itaambatanishwa na muhtasari wa kikao hiki kwenda Ofisi ya Mratibu Elimu Kata ili waweze kujadiliwa kwenye kikao cha kamati ya maendeleo ya Kata kwa msaada zaidi.
DONDOO NA 7. KUSOMA NA KUJADILI BARUA YA MAOMBI YA KUMILIKISHWA SILAHA.
Dondoo hii haikuzungumzwa kwa sababu yakutokuwepo kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Kivule Ndugu Juliaus M. Gekula ambaye ni mwakilishi wa mw/ kiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wa Kata ya Kivule..
DONDOO NA8. KUJADILI NAMNA YA KUDHIBITI MALORI YA MCHANGA YANAYO PITA NDANI YA MTAA WA KIVULE.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule aliwaonyesha wajumbe stakabadhi zinazo tolewa na Mtaa wa Mbondole za kulipia kwa ajili ya wanaopitisha malori ya mchanga katika maeneo ya barabara za Mtaa huo.Kwa kauli moja waliazimia kuwa mawazo hayo yapelekwe kwenye mkutano wa wananchi wa Mtaa walijadili na maamzi yapelekwe katika kikao cha KMK kwa utekelezaji zaidi.  
DONDOO NA 9. KUFUFUA STENDI NA SOKO LA MTAA WA KIVULE.
M/kiti wa S/kali ya Mtaa wa Kivule aliwaeleza wajumbe kuwa umuhimu wa kufufua stendi na soko,ni kwa ajili ya maendeleo ya Mtaa huu wa Kivule..
Wajumbe waliunga mkono dondoo hiyo na kusema stendi na soko vikifanya kazi tutapata faida zifuatazo:
a)    Wananchi wote wa Mtaa wa Kivule na Mitaa jirani wataweza kupata huduma ya usafiri wa uhakika.
b)    Kufanya soko kuchangamka ili wajasiriamali wa ndani na nje ya Mtaa wa Kivule kufanya biashara za uhakika na kutoa huduma.nzuri kwa wakazi.wetu.
c)    Wanachi wa Mtaa wa Kivule, wakiwemo vijana,akina mama nk.watapata ajira nakupunguza umaskini ndani ya Mtaa wetu.
d)    Maeneo hayo ya Stendi na Soko yatakuwa yametimiza matarajio ya matumizi na mipango ya wananchi, S/kali pamoja na wadau waliotoa maeneo hayo ili yatumike kama yalivyo pangiliwa na mikutano/vikao mbalimbali hata kabla ya ndoto za Kata hii kuwepo. kutokana na faida hizo mtaa utaweza kujitegemea kiuchumi.
         DONDOO NA 10. KUPANGA TAREHE NA DONDOO ZA MKUTANO HUO.
Wajumbe katika kikao hicho walikubaliana kuwa mkutano wa mtaa ufanyike tarehe 30/03/2013, muda wa saa 8.00 mchana ndani ya uwanja wa S/kali ya Mtaa.
 kikao cha kukutana na wajumbe wa kamati za siasa za matawi saba ya CCM yaliopo ndani ya Mtaa huu, wajumbe wameazimia kifanyike tarehe 16/03/2013 saa 8.00 mchana katika Tawi la Magole A. Kikao hicho ni kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa tarehe 30/03/2013 kikatiba.
NB;Wajumbe waliomba matangazo ya mikutano/vikao iweinatolewe mapema iwezekanavyo. Kwa viongozi wote wa Kanda na Matawi.
DONDOO NA 11. KARAKANA BUBU ENEO LA A MTAA WA KIVULE.
Wajumbe wameona ni muhimu sasa karakana bubu iliyopo kwenye eneo la STENDI ya Kivule kwa namna yeyote ile ihamishwe ili eneo hilo liwe wazi kwa ajili ya huduma ya ABIRIA na si vinginevyo.
Baada ya mjadala mrefu wa dondoo hii, wajumbe wa kikao waliazimia kuwa;.
a)    Mmiliki wa karakana hiyo aandikiwe barua ya kumtaka ahame katika eneo hilo mara moja kama alivyoingia, kabla ya lazimisho la KISHERIA kuchukua mkondo wake.
b)    Barua hiyo inakiliwe kwa VIONGOZI wafuatao kwa taarifa;
                      I.        Afisa Mtendaji Kata Kivule------------------------------Taarifa
                    II.        M/kiti wa Baraza la Kata ya Kivule--------------------Taarifa kwa SHERIA zaidi.
                   III.        Afisa Afya Kata ya Kivule--------------------------------Taarifa kwaMazingira.
DONDOO NA 13. KUFUNGA KIKAO.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa kivule alitoa shukrani kwa wajumbe waliyo hudhuria kwa michango yao ya kina na maazimio yenye mwelekeo ya kuimarisha maendeleo ya Mtaa wa Kivule.
Alifunga kikao saa 6:58 mchana.

                                                                    


No comments:

Post a Comment