Sunday, March 17, 2013

Wanafunzi Kivule watozwa nauli sh 300


habari iliyotoka 29 februari 2012
WAKAZI wa Kata ya Kivule, jijini Dar es Salaam, wamelalamikia kitendo cha madereva wa daladala kuwatoza wanafunzi sh. 300 kwa kisingizio cha ubovu wa barabara.
Wakizungumza katika kikao cha kuchangia ununuzi wa Kivuko cha Kipunguni Mtaa wa Mara Picknic kilichoitishwa na Diwani wa Kivule, Nyansika Gaitama, wakazi hao walisema hali hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza kusababisha wazazi kushidwa kupeleka watoto wao shule.
Kutokana na hali hiyo, mmoja wa wakazi hao Mwalimu Mulokozi aliitaka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), kupeleka watendaji wake huko ili kujionea hali halisi badala ya kubaki maofisini.
Katika uchangishaji wa kivuko, jumla ya sh milioni 3.6 zilipatikana ambapo kati ya hizo Diwani alichangia sh.100,000.
Diwani Gaitama alisema kukamilika kwa kivuko hicho kutawezesha barabara hiyo kupitika hadi kipidi cha mvua.
Hata hivyo, alisema zinahitajika sh milioni 11.6 ili kukamilika kwa ujenzi wa kivuko hicho ambapo alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza kuchangia.


No comments:

Post a Comment