Blog hii inamilikiwa na Serikali ya Mtaa wa Kivule, Madhumuni ya Blog hii ni kuweka bayana habari zote zinazojitokeza katika mtaa wetu wa Kivule, pia watu watapata nafasi ya kuona maendeleo ya mtaa wetu. Wafanya biashara wote watakuwa na nafasi ya kutangaza biashara zao kupita blog hii.
RAIS KIKWETE ATEMBELEA JENGO LILILOPOROMOKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zilikuwa zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam
Baadhi ya picha baada ya kuporomomoka kwa jengo linalokadiliwa kuwa lenye ghorofa 16 lililokuwa bado linaendelea kujengwa katika makutano ya barabara ya Indira Gandhi na Morogoro Road
No comments:
Post a Comment